2 John

Salamu

1 aMzee:

Kwa bibi mteule na watoto wake, niwapendao katika kweli, wala si mimi tu, bali na wale wote waijuayo kweli:
2 bkwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itaendelea kukaa nasi milele:

3 cNeema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Isa Al-Masihi, Mwanawe Baba, itakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.

Kweli Na Upendo

4Imenipa furaha kuu kuona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile Baba alivyotuagiza. 5 dSasa, bibi mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.Tupendane kila mmoja na mwenzake. 6 eHili ndilo pendo, kwamba tuenende sawasawa na amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo.

7 fWadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Isa Al-Masihi amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na anampinga Al-Masihi. 8 gJihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu. 9 hMtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Al-Masihi, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. 10 iMsimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. 11 jYeyote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.

Salamu Za Mwisho

12 kNinayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.

13 lWatoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amen.
Copyright information for SwhKC